Rais
mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa amewataka wadau wote wa
maendeleo ya mkoa wa Mtwara kusitisha harakati zao za maandamano na mihadahara
ya kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es salaam na badala
yake kukaa pamoja kujadili suala hilo
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari,imemnukuu rais Mkapa akizitaka pande zote kushirikiana kwa pamoja
kupitia historia,kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wa mradi huo na na
kufikia muafaka wa ujia wa maendeleo
Rais
Mkapa amesema fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano kamwe si masharti ya
maendeleo bali mazungumzo yataboresha sera, ya uwekezaji ya mkoa na nchi kwa
ujumla.
Amesema
vituko na kauli za hivi karibuni kutoka kwa wananchi na viongozi wa vyama vya
siasa zimekaribia kujenga kutokuelewana
kati ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali, kati ya wanachama wa vyama vya
siasa na viongozi wao, kati ya wananchi na viongozi wa Serikali.
Ameongeza
kuwa Mtafaruku huu haufai kuachwa uendeleee na kutishia usalama kwa kuwa
mipango, Mikakati na mbinu za Utekelezaji wa maendeleo siyo siri na
kwamba maelezo yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi
ambayo raslimali zitawanufaisha wananchi wa eneo hilo
No comments:
Post a Comment