![]() |
Herve Renard |
Baada ya kushuhudia timu yake ikiondolewa katika
michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu, kocha mkuu wa Zambia Herve
Renard amesema anajua fika kuwa shirikisho la soka Afrika Caf litakuwa na
furaha baada ya waliokuwa mabingwa hao watetezi kuondolewa katika hatua ya
makundi.
Renard amesema Caf walikuwa hawapendi kuona Zambia
ikitetea ubingwa huo na hatimaye kushiriki kombe la mabara nchini Brazil kwa
kuwa wanaamini kuwa Chipolopolo haichezi soka la kuvutia.
Kocha huyo raia wa Ufaransa ameongeza na kusema kuwa
kutolewa kwao sio mwisho wa dunia hivyo wanatakiwa wajipange katika michuano
ijayo.
Naye mlinda mlango wa Zambia Kennedy Mweene amewataka
wachezaji wenzake wazidi kushikama katika kipindi hiki ili waweze kufanya
vizuri katika michezo ya kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2014
nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment