Karibu katika blog yetu

Saturday, November 24, 2012

HAYATOU APONGEZA JITIHADA ZA CECAFA

Rais wa CAF Issa Hayatou.
Rais wa Shirikisho la soka Afrika, CAF, Issa Hayatou amesifu jitihada za baraza la michezo la Afrika mashariki CECAFA kwa jitihada zake za kuhakikisha mchezo wa kandanda unakua katika ukanda huu.
Hayatou amesema kuwa anaheshimu sana jitihada za baraza hili na ndio maana alikubali mwaliko wa kushuhudia ufunguzi wa fainali za michuano hii licha ya kuwa na shughuli nyingine muhimu.
Ameyataka mashirikisho mengine kuiga mfano wa CECAFA katika kuhakikisha maendeleo yanakuza maendeleo ya soka katika kanda zao.


Monday, November 12, 2012

WANYAMA NA OLIECH WAITWA KUIVAA TAIFA STARS


TIMU ya taifa ya Kenya, Harambee Stars inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza leo kesho (Jumanne) saa 2:30 asubuhi, ikiwa na wachezaji wake nyota tayari kwa pambano la kirafiki la kimataifa litakalofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huo, unaochezwa siku ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA), itakuwa ya pili ya majaribio kwa Stars ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D la michuano ya awali ya Kombe la Dunia.

Katika mechi ya kwanzaya kirafiki mwaka huu, Stars ililazimisha sare ya mabao 3-3 na Botswana katika mchezo uliofanyika jijini Gabarone.
Harambee Stars.
Kenya, ambayo inashika nafasi ya 130 kwenye orodha ya ubora ya FIFA, inakuja na wachezaji wake nyota akiwemo mshambuliaji hatari Victor Mugubi Wanyama ambaye wiki iliyopita alifunga moja ya mabao mawili wakati Barcelona ilipozamishwa kwa mabao 2-1 na Celtic ya Scotland.

Kocha Mfaransa Henry Louis Michel pia amemjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji hatari wa Auxerre ya Ufaransa, Dennis Oliech ambaye pia ni nahodha, Ayub Timbe Masika, ambaye anachezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, beki beki Brian Mandela wa Santos ya Afrika Kusini na kipa Anord Origi Otieno anayechezea klabu ya Ull/Kisa ya Norway.

Pamoja na nyota hao kutoka nje, Harambee Stars pia inaundwa na wachezaji wengi wanaochezea klabu kubwa za Kenya, zikiwemo Tusker, Sofapaka, Mathare United na Gor Mahia.

Kikosi kamili cha Harambee Stars kinaundwa na Arnold Orig Otieno,  Dennis Oliech, Victor Mugubi Wanyama, Ayub Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos), Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).

Wengine ni Geofrey Kokoyo Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma (Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba,  Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.

Viongozi ni kocha Henry Louis Michel akisaidiwa na Mohammed Ajam Boujarari, Florent Louis Robert Motta, Sunil Shah, Wycliff Obiero Makanga, Wilberforce Bruce Juma, Benson Kennedy Otieno, Ali Abdallah Rehan, Robert Asembo Akumu na Angeline Mwikali Nzavi

Friday, November 9, 2012

BANDA: ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA KUHIMIZA UMUHIMU WA UVUMILIVU WA KISIASA

ALIYEKUWA rais wa Zambia kuanzia mwaka 2008 mpaka 2011 akichukua madaraka mara baada ya kifo cha levy Mwanawasa, Rupiah Banda amesema kuwa uvumilivu wa kisiasa ndio suala muhimu katika nchi yoyote duniani.

Banda amesema hayo wakati akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa alipokuwa katika ziara ya kutembekea chuo hicho kikongwe barani Afrika.

Kiongozi huyo wa Zambia ambaye baada ya kushindwa Urais na kiongozi wa chama cha upinzani cha nchi hiyo Michael Sata mwaka 2011 aliondoka madarakani bila matatizo huku akikubali kushindwa na kuwataka wananchi wa Zambia wakiwemo wafuasi wa chama chake kuwa kitu kimoja na serikali mpya ya nchi hiyo katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Zaambia iliyopo kusini mwa Afrika.

Katika mazungumzo yake na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Banda amekiri kuwa kuna baadhi ya wafuasi wake walikuwa wanamtaka agomee matokeo na kukataa kushindwa lakini hakutaka kufanya hivyo kwani aliamini ameshindwa kihalali na hakukuwa na sababu ya kufanya maamuzi ambayo yangeiingiza Zambia katika machafuko na ghasia.

Katika hatua nyingine Banda amempongeza mshambuliaji wa soka wa Tanzania anayecheza soka katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta kwa kiwango chake na amesema kuw amchezaji huyo atafika mbali.

Ukiachilia mbali masuala ya siasa, Banda ni mshabiki mkubwa wa mchezo wa kandanda na kwa sasa ni mwenyekiti wa mashabiki wa timu ya taifa ya nchi hiyo Chipolopolo.

Thursday, November 8, 2012

PROF. KILLIAN AWATAKA WANASISA NCHINI KUWA NA ITIKADI INAYOELEWEKA

MHADHIRI mwandamizi wa masuala ya uongozi na siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa duniani Professor Bernadetta Killian amewataka wanasiasa kuhakikisha wanakuwa na sera na itakadi zinazoelewaka wakati wakiwa wanajinadi katika majukwaa ili wapigiwe kura kushika nyadhifa mbalimbali.

Prof. Bernadeta Killian
Prof. Killian amesema hayo wakati akiongea na Mlimani TV na kuongeza kuwa Rais mteule wa Marekani Barack Obama ameshinda kwa mara nyingine tena kutokana na kuwa na sera na mlengo unaoelewaka kiasi cha kuweza kuwashawishi vijana na wanawake wengi kumpigia kura na hatimaye kumshinda mpinzani wake wa chama cha Republican Mitt Romney.

HU JINTAO AAHIDI MABADILIKO YA KISIASA NCHINI CHINA

WAKATI serikali ya Jamuhuri ya watu wa China ikiwa katika kipindi cha mabadiliko ya uongozi wa juu wa nchi hiyo, Rais anayemaliza muda wake Hu Jintao ameahidi mabadiliko ya mfumo wa kisiasa ambao utatoa fursa zaidi kwa vijana wa nchi hiyo kuweza kushika nafasi za juu katika dola ya nchi hiyo iliyopiga hatua kubwa kiuchumi kuliko nchi yoyote kwa sasa duniani.

Mfumo wa kisiasa wa China ambao ni wa chama cha Kikomunisti umekuwa ukionekana kuwabana zaidi vijana wa nchi hiyo kuchagua na kushika nafasi za utawala.

Katika hatua nyingine Hu Jintao amekiri kuwa suala la rushwa litakimaliza chama hicho endapo kama wanachama na viongozi wa chama hicho hawataondokana na tatizo hilo.