Karibu katika blog yetu

Friday, December 7, 2012

MNYIKA ASHINDA KESI YA UBUNGE - UBUNGO


Mhe. John Mnyika ambaye kwa sasa tangu kutangazwa kwa shauri hilo, ni mbunge halali wa jimbo la Ubungo mara tu baada ya kutoka makamani hapo, na kuongea na wananchi kupitia vyombo vya habari, huku wanaomzunguka wakiwa ni wafuasi wa chama hicho.

Na Amini Mgheni
MAHAKAMA ya rufaa imetupilia mbali rufani dhidi ya ubunge wa jimbo la ubungo, ambapo awali waliofungua kesi hiyo alieyekuwa mgombea kupitia chama cha mapinduzi, waliwasilisha dhamira yao mbele ya mahakama hiyo ya kutaka kufutwa kwa kesi hiyo kulingana na ridhaa yao wenyewe.

Kama mwandishi wa mtandao huu napata fursa ya kukutana na Mhe. John Mnyika baada ya shauri la kesi hiyo kumalizika naye akaeleza jinsi kesi hiyo ilivyomalizika.

‘‘Masuala ya kesi dhidi ya ubunge wetu, na kura zetu tulizopiga leo ndo yaamefikia hatma, kwahiyo hakuna tena kupingwa kwa namna yeyote ile, jambo hili limemalizika na sasa tunaweza kuendelea na kazi bila kuwa na kesi au mashauri yeyote mahakamani’’ alisema Mhe. John Mnyika

Mhe. John Mnyika akiongea na wananchi waliofika mahakamani hapo kusikiliza shauri hilo.
Kwa muda mrfu mbunge wa jimbo la ubungo amekuwa akiendelea kufanya kazi licha ya mapingamizi kadha wa kadha ambayo yote ameshinda.

Lakini pia kama mwandishi wa mtandao huu wa mlimanimedia.blogspot.com nikataka kujua endapo kesi hii imeondolewa katika ngazi ya rufaa, je watadai fidia kama kesi nyingine wanavyofanya? Mnyika akawa na haya ya kuzungumza;

‘‘Tukubali kwamba kama wametoa kesi katika ngazi ya rufaa basi nasisi tusamehe’’ alisema Mnyika.


Baadhi ya wakereketwa wa CHADEMA wakishangilia baada ya Mhe. John Mnyika kushinda kesi hiyo.
Kufutwa kwa kesi hiyo kunafanya ubunge wa jimbo la ubungo kutokuwa na shaka yeyote, ambapo mpaka hivi sasa hakuna kesi yeyote mahakamani, jambo linalotoa fursa kwa mbunge huyo kutekeleza majukumu yake mengine ya kitaifa kama alivyowaahidi wananchi wa jimbo la ubungo.