Karibu katika blog yetu

Friday, February 1, 2013

SUPER EAGLES YAPATA MOTISHA



                                                         
Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria wamepokea kiasi cha dola 30,000 kila mmoja kutoka shirikisho la soka la nchi hiyo kwa kufanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Fedha hizo zimetolewa na shirikisho la soka la Nigeria NFF ili kuwapa motisha wachezaji kushinda katika mchezo wake unaofuata dhidi ya Ivory Coast unaotarajiwa kuchezwa wikend hii.

Toka ianze michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Nigeria imeshiriki michuano hiyo mara 17 na imefanikiwa kusonga mbele mara 15.


Wakati Nigeria wakipokea kiasi hicho cha fedha, Ghana wamepokea dola 5000 kila mmoja kwa kuingia hatua hiyo ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment