Karibu katika blog yetu

Monday, November 12, 2012

WANYAMA NA OLIECH WAITWA KUIVAA TAIFA STARS


TIMU ya taifa ya Kenya, Harambee Stars inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza leo kesho (Jumanne) saa 2:30 asubuhi, ikiwa na wachezaji wake nyota tayari kwa pambano la kirafiki la kimataifa litakalofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huo, unaochezwa siku ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA), itakuwa ya pili ya majaribio kwa Stars ambayo inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D la michuano ya awali ya Kombe la Dunia.

Katika mechi ya kwanzaya kirafiki mwaka huu, Stars ililazimisha sare ya mabao 3-3 na Botswana katika mchezo uliofanyika jijini Gabarone.
Harambee Stars.
Kenya, ambayo inashika nafasi ya 130 kwenye orodha ya ubora ya FIFA, inakuja na wachezaji wake nyota akiwemo mshambuliaji hatari Victor Mugubi Wanyama ambaye wiki iliyopita alifunga moja ya mabao mawili wakati Barcelona ilipozamishwa kwa mabao 2-1 na Celtic ya Scotland.

Kocha Mfaransa Henry Louis Michel pia amemjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji hatari wa Auxerre ya Ufaransa, Dennis Oliech ambaye pia ni nahodha, Ayub Timbe Masika, ambaye anachezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, beki beki Brian Mandela wa Santos ya Afrika Kusini na kipa Anord Origi Otieno anayechezea klabu ya Ull/Kisa ya Norway.

Pamoja na nyota hao kutoka nje, Harambee Stars pia inaundwa na wachezaji wengi wanaochezea klabu kubwa za Kenya, zikiwemo Tusker, Sofapaka, Mathare United na Gor Mahia.

Kikosi kamili cha Harambee Stars kinaundwa na Arnold Orig Otieno,  Dennis Oliech, Victor Mugubi Wanyama, Ayub Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos), Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).

Wengine ni Geofrey Kokoyo Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma (Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba,  Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.

Viongozi ni kocha Henry Louis Michel akisaidiwa na Mohammed Ajam Boujarari, Florent Louis Robert Motta, Sunil Shah, Wycliff Obiero Makanga, Wilberforce Bruce Juma, Benson Kennedy Otieno, Ali Abdallah Rehan, Robert Asembo Akumu na Angeline Mwikali Nzavi

No comments:

Post a Comment