Karibu katika blog yetu

Friday, November 9, 2012

BANDA: ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA KUHIMIZA UMUHIMU WA UVUMILIVU WA KISIASA

ALIYEKUWA rais wa Zambia kuanzia mwaka 2008 mpaka 2011 akichukua madaraka mara baada ya kifo cha levy Mwanawasa, Rupiah Banda amesema kuwa uvumilivu wa kisiasa ndio suala muhimu katika nchi yoyote duniani.

Banda amesema hayo wakati akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa alipokuwa katika ziara ya kutembekea chuo hicho kikongwe barani Afrika.

Kiongozi huyo wa Zambia ambaye baada ya kushindwa Urais na kiongozi wa chama cha upinzani cha nchi hiyo Michael Sata mwaka 2011 aliondoka madarakani bila matatizo huku akikubali kushindwa na kuwataka wananchi wa Zambia wakiwemo wafuasi wa chama chake kuwa kitu kimoja na serikali mpya ya nchi hiyo katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Zaambia iliyopo kusini mwa Afrika.

Katika mazungumzo yake na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Banda amekiri kuwa kuna baadhi ya wafuasi wake walikuwa wanamtaka agomee matokeo na kukataa kushindwa lakini hakutaka kufanya hivyo kwani aliamini ameshindwa kihalali na hakukuwa na sababu ya kufanya maamuzi ambayo yangeiingiza Zambia katika machafuko na ghasia.

Katika hatua nyingine Banda amempongeza mshambuliaji wa soka wa Tanzania anayecheza soka katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta kwa kiwango chake na amesema kuw amchezaji huyo atafika mbali.

Ukiachilia mbali masuala ya siasa, Banda ni mshabiki mkubwa wa mchezo wa kandanda na kwa sasa ni mwenyekiti wa mashabiki wa timu ya taifa ya nchi hiyo Chipolopolo.

No comments:

Post a Comment