TIMU ya taifa ya Kenya, Harambee
Stars inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza leo kesho (Jumanne) saa 2:30 asubuhi,
ikiwa na wachezaji wake nyota tayari kwa pambano la kirafiki la kimataifa
litakalofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo huo, unaochezwa siku ya
mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu
(FIFA), itakuwa ya pili ya majaribio kwa Stars ambayo inashika nafasi ya pili
kwenye Kundi D la michuano ya awali ya Kombe la Dunia.
Katika mechi ya kwanzaya kirafiki
mwaka huu, Stars ililazimisha sare ya mabao 3-3 na Botswana katika mchezo
uliofanyika jijini Gabarone.
 |
Harambee Stars. |
Kenya, ambayo inashika nafasi ya
130 kwenye orodha ya ubora ya FIFA, inakuja na wachezaji wake nyota akiwemo mshambuliaji
hatari Victor Mugubi Wanyama ambaye wiki iliyopita alifunga moja ya mabao
mawili wakati Barcelona ilipozamishwa kwa mabao 2-1 na Celtic ya Scotland.
Kocha Mfaransa Henry Louis Michel
pia amemjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji hatari wa Auxerre ya
Ufaransa, Dennis Oliech ambaye pia ni nahodha, Ayub Timbe Masika, ambaye
anachezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, beki beki Brian Mandela wa Santos ya
Afrika Kusini na kipa Anord Origi Otieno anayechezea klabu ya Ull/Kisa ya
Norway.
Pamoja na nyota hao kutoka nje,
Harambee Stars pia inaundwa na wachezaji wengi wanaochezea klabu kubwa za
Kenya, zikiwemo Tusker, Sofapaka, Mathare United na Gor Mahia.
Kikosi kamili cha Harambee Stars
kinaundwa na Arnold Orig Otieno, Dennis
Oliech, Victor Mugubi Wanyama, Ayub Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos),
Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango
Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).
Wengine ni Geofrey Kokoyo
Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma
(Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba, Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew
Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.
Viongozi ni kocha Henry Louis Michel akisaidiwa
na Mohammed Ajam Boujarari, Florent Louis Robert Motta, Sunil Shah, Wycliff
Obiero Makanga, Wilberforce Bruce Juma, Benson Kennedy Otieno, Ali Abdallah
Rehan, Robert Asembo Akumu na Angeline Mwikali Nzavi