Na Amini Mgheni
MAHAKAMA ya rufaa imetupilia mbali rufani dhidi ya ubunge wa jimbo la ubungo, ambapo
awali waliofungua kesi hiyo alieyekuwa mgombea kupitia chama cha mapinduzi,
waliwasilisha dhamira yao mbele ya mahakama hiyo ya kutaka kufutwa kwa kesi
hiyo kulingana na ridhaa yao wenyewe.
Kama mwandishi
wa mtandao huu napata fursa ya kukutana na Mhe. John Mnyika baada ya shauri la
kesi hiyo kumalizika naye akaeleza jinsi kesi hiyo ilivyomalizika.
‘‘Masuala
ya kesi dhidi ya ubunge wetu, na kura zetu tulizopiga leo ndo yaamefikia hatma, kwahiyo hakuna tena kupingwa kwa namna yeyote ile, jambo hili limemalizika na
sasa tunaweza kuendelea na kazi bila kuwa na kesi au mashauri yeyote
mahakamani’’ alisema Mhe. John Mnyika
![]() |
Mhe. John Mnyika akiongea na wananchi waliofika mahakamani hapo kusikiliza shauri hilo. |
Kwa
muda mrfu mbunge wa jimbo la ubungo amekuwa akiendelea kufanya kazi licha ya
mapingamizi kadha wa kadha ambayo yote ameshinda.
Lakini pia kama mwandishi wa mtandao huu wa mlimanimedia.blogspot.com nikataka kujua endapo kesi hii imeondolewa katika ngazi ya rufaa, je watadai
fidia kama kesi nyingine wanavyofanya? Mnyika akawa na haya ya kuzungumza;
‘‘Tukubali kwamba kama wametoa kesi katika ngazi ya rufaa basi nasisi
tusamehe’’ alisema Mnyika.
![]() |
Baadhi ya wakereketwa wa CHADEMA wakishangilia baada ya Mhe. John Mnyika kushinda kesi hiyo. |
Kufutwa
kwa kesi hiyo kunafanya ubunge wa jimbo la ubungo kutokuwa na shaka yeyote,
ambapo mpaka hivi sasa hakuna kesi yeyote mahakamani, jambo linalotoa fursa kwa
mbunge huyo kutekeleza majukumu yake mengine ya kitaifa kama alivyowaahidi wananchi wa
jimbo la ubungo.